SUDANI KUSINI-SIASA

Sudan Kusini yataka kutunza amani na usalama

Rais wa Sudan Salva Kiir na makamu wake Riek Machar..
Rais wa Sudan Salva Kiir na makamu wake Riek Machar.. REUTERS/Jok Solomun

Sudan Kusini imeanza mchakato wa kuandika katiba mpya, itakayosaidia kuimarisha amani nchini humo baada ya karibu miaka 10 ya vita tangu ilipopata uhuru wake mwaka 2011.

Matangazo ya kibiashara

Mchakato huu ulizinduliwa na rais Salva Kiir ni miongoni mwa makubaliano kwenye mkataba uliosainiwa mwaka 2018 kati yake na kiongozi wa upinzani Riek Machar ambaye sasa ni Makamu wa Kwanza wa rais.

Tangu ilipapata uhuru wake na kujitenga na Sudan mwaka 2011 na katika kipindi chote cha vita, taifa hilo chnaga duniani, limekuwa likiongozwa na Katiba za mpito.

Iwapo mchakato huu utamalizika na kukubaliwa na pande zote, basi nchi hiyo sasa itakuwa na katiba dhabiti inayotarajiwa kusaidia kuleta amani ya kudumu nchini Sudan Kusini.

Mchakato huu unaanza wakati huu wachambuzi wa siasa za Sudan Kusini wakionya kuwa huenda nchi hiyo ikarejea kwenye vita iwapo makubaliano yote ya mkataba wa amani hayataheshimiwa na pande mbili.

Inaelezwa kuwa mchakato huu unatarajiwa kumalizika baada ya miaka miwili.