BURUNDI-USALAMA

Watu kadhaa wauawa katika milipuko ya guruneti mjini Bujumbura

Watu wasiojulikana walirusha guruneti katika maeneo mbalimbali jijini BUjumbura, watu kadhaa waliuawa na wengine weni kujeruhiwa.
Watu wasiojulikana walirusha guruneti katika maeneo mbalimbali jijini BUjumbura, watu kadhaa waliuawa na wengine weni kujeruhiwa. AFP/File

Hali ya wasiwasi imetanda jijini Bujumbura baada ya watu wasiojulikana kuvurumisha guruneti katika maeneo mbalimbali ikiwemo kituo cha basi katika jiji kuu. Watu kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha, huku wengine wakijeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo mbali mbali vimeripoti kuwa mashambulio 4 ya guruneti yalitekelezwa jioni ya Jumanne, karibu saa moja usiku, katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo la Bujumbura, ambapo gurunedi zilivurumishwa katika maegesho ya mabasi kwenye soko la Ngagara, linalojulikana kama "Cotebu". na kuwaua watu 4, huku wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mtu anayedaiwa kurusha gurunedi hilo alipigwa risasi na polisi, kulingana na mashuhuda waliokuwepo, wakisema kuwa mhalifu huyo alikuwa na mabomu mengine.

Mashambulio mengine ya guruneti yaliripotiwa katika maegesho ya mabasi eneo la"Plazza ”, Magharibi mwa soko kuu la zamani la Bujumbura, mbele ya mabanda ya wauzaji wa mboga.

Shambulio lingine la guruneti lilitekelezwa kwenye barabara kuu ya Boulevard du Peuple Murundi, katika eneo la Bwiza, kwenye maegesho ya basi inayoitwa "Kudumu".

Madaktari katika hospitali ya Prince Regent Charles wanaripotiwa kuwa walizidiwa baada ya kupokea mamia ya watu waliojeruwa.