TANZANIA-SIASA

Upinzani waanza kukutana na wafuasi wao katika utawala wa Samia Suluhu Hassan

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzai nchini Tanzania, CHADEMA, Freeman Mbowe,.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzai nchini Tanzania, CHADEMA, Freeman Mbowe,. Screenshot Youtube

Vyama vya upinzani nchini Tanzania, vinaonekana kuanza kujihusisha na harakati za kisiasa, chini ya uongozi wa rais Samia Suluhu Hassan.

Matangazo ya kibiashara

 Kwa zaidi ya miaka mitano wanasiasa wa upinzani hawakuweza kukutana na wafuasi wao baada ya aliyekuwa rais Hayati John Magufuli kupiga marufu mikutano ya siasa hadi wakati wa uchaguzi mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA, Freeman Mbowe ameonekana hivi karibuni akikutana na wafuasi wa chama hicho katika maeneo mbalimbai nchini humo.

Katika utawala wa Hayati John Pombe Maufuli,  ulikuwa ukisema katika kuwa « Tanzania hivi sasa ina mmomonyoko wa demokrasia na kuna ishara zote za utawala wa udikteta, usiojali haki za kisiasa, kijamii pamoja na za kiuchumi kwa wananchi ».

Wapinzani hao walisema serikali ya rais Magufuli imekuwa ikiendeleza vita dhidi ya vyama vya upinzani pamoja na wote wanaonekana wana mawazo mbadala juu ya namna « nchi yetu inavyoendeshwa », ingawa katiba ya nchi inalinda mfumo wa vyama vingi.

Mara tu baada ya kuingia madarakani mwaka 2015 serikali ya Rais Magufuli ilipiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ikisema kwamba muda wa kampeni umekwisha.