RWANDA-HAKI

Rwanda: Mkosoaji wa serikali ya Rwanda kupitia mtandao wa You Tube akamatwa

Katika video yake ya YouTube, Aimable Karasira amekuwa akiikosoa serikali ya Rwanda kwa miezi kadhaa na ametoa maneno yanayozua utata nje na ndani ya nchi hiyo.
Katika video yake ya YouTube, Aimable Karasira amekuwa akiikosoa serikali ya Rwanda kwa miezi kadhaa na ametoa maneno yanayozua utata nje na ndani ya nchi hiyo. © AFP

Aimable Karasira, profesa wa zamani wa chuo kikuu aliyeachishwa kazi hivi karibuni, anatuhumiwa kukana mauaji ya Watutsi. Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda ilitangaza kukamatwa kwake Jumatatu jioni, kwenye Twitter.

Matangazo ya kibiashara

Katika video yake ya YouTube, Aimable Karasira amekuwa akiikosoa serikali ya Rwanda kwa miezi kadhaa na ametoa maneno yanayozua utata nje na ndani ya nchi hiyo. Anazungumza mara kwa mara juu ya mauaji ya kimbari ya Watutsi na uhalifu uliofanywa na Chama cha Patriotic Front, kinachotawala Rwanda kwa sasa.Katika video yake ya mwisho iliyochapishwa Mei 20, alilinganisha Rwanda ya Paul Kagame na Korea Kaskazini. Anadai kuwa ni mmoja wa manusura wa mauaji ya kimbari na anashtumu askari wa RPF kwa kuwaua wazazi wake.

"Karasira anaonekana mara kwa mara akizungumzia juu ya mauaji ya Watutsi, akisema kwamba hayakupangwa," Ofisi ya Upelelezi ya Rwanda ilisema kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu, na kuongeza kuwa mtu yeyote anayetenda uhalifu kwenye mitandao ya kijamii ataadhibiwa.

Mnamo mwezi Februari mwaka huu, Yvonne Idamange, Mtumiaji wa mtandao wa YouTube ambaye alikosoa hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya janga la Corona na ambaye alihakikisha kwamba Rais Paul Kagame aliaa dunia, pia alikamatwa.

Wakati Wanyarwanda wanaendelea kwa wingi kutumia mitandao ya kijamii kujieleza, angalau waandishi wa habari sita au watoa maoni kwenye mtandao wamewekwa kizuizini, wamekamatwa au kushtakiwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.