KENYA SOMALIA DIPLOMASIA

Kenya yarejesha uhusiano wake wa kidiplomasia na Somalia

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed (L) na mwenzake wa Kenya, Uhuru Kenyatta, wamipokutana Nairobi mnamo Machi 2017.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed (L) na mwenzake wa Kenya, Uhuru Kenyatta, wamipokutana Nairobi mnamo Machi 2017. AFP - SIMON MAINA

Baada ya mvutano wa takriban miezi sita kati ya Kenya na Somalia, uhusiano wa kidiplomasia umerejea tena baada ya mawasiliano tulivu baina ya mawaziri wa mambo ya nnje kutoka mataifa hayo mawili. Jumamosi, Juni 12, Mogadishu ilikuwa imeashiria kwamba inataka kufungua tena ubalozi wake jijini Nairobi. Mualiko ulikubaliwa Jumatatu, Juni 14 na Nairobi, ambayo imeona kwamba itakuwa verma hilo lifanytike haraka iwezekanavyo.

Matangazo ya kibiashara

Uhusiano kati ya Kenya na Somalia umekuwa katika mgogoro mkubwa kwa karibu miaka miwili na nusu, baada ya Mogadishu kupiga mnada sehemu za mafuta katika eneo la bahari linalodaiwa na Nairobi. licha ya hatuwa hiyo ya kurejea kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili, mizizi ya mgogoro bado iko.

Mzozo wa mpaka ambao haujasuluhishwa

Nchi hizo mbili bado hazijasuluhisha mzozo wao wa mpaka. Hukumu ya mahakama ya Haki ya Kimataifa inasubiriwa, wakati Kenya iliepuka vikao vya mwisho mnamo Machi kwa kuishutumu ICJ kwa upendeleo.

Katika muktadha huu, sio hakika kwamba uamuzi wa majaji unasuluhisha kabisa mzozo. Masuala mengine pia yanasubiri. Majadiliano ya kibiashara lazima yafanyike, haswa juu ya marufuku ya Somalia juu ya khat ya Kenya na juu ya ufikiaji wa kampuni ya Kenya Airways kwenda uwanja wa ndege wa Mogadishu.

Mwishowe, kuna swali la kambi ya Dadaab. Kenya inataka ifungwe. Kurudi kwa wakimbizi karibu 500,000, haswa Wasomali, imepangwa Juni 2022. Haya ni maswala ya mwiba yanayoweza kufufua mvutano wa pande zote wakati wowote.

"Kufungua tena" kwa ubalozi

Wakati huo huo, serikali ya Kenya "itafungua tena ubalozi wake huko Mogadishu haraka iwezekanavyo" na "inakaribisha balozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia kurudi Nairobi na kuanza tena kazi zake".