BURUNDI - HABARI

Burundi: vikwazo dhidi ya vyombo vya habari BBC na Ikiriho vyaondolewa

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye AFP Photos/Tchandrou Nitanga

Baraza la kitaifa linalofuatilia vyombo vya habari nchini Burundi, CNC limetangaza kuondolewa kwa vikwazo ilivyokuwa imevika kwa shirika la utangazaji habari kutoka Uingereza BBC kusikika nchini Burundi pamoja na Gazeti la Ikiriho kuanzia  Jumatano Juni 16, 2021,

Matangazo ya kibiashara

Baada ya majadiliano, wajumbe wa Bodi ya Utendaji ya CNC walibaini kuwa hakukuwa na kikwazo kwa Shirika la habari la Uingereza BBC kusikika nchini Burundi itabidi taasisi hiyo kuwasilisha ombi jipya la leseni ya uendeshaji kwa maendeleo mazuri ya utaratibu," alisema Laurent Kaganda, makamu -Rais wa chombo hiki cha kudhibiti vyombo vya habari katika taarifa kwa waandishi wa habari.

Hatua hii inafuata mwito wa Januari 28, 2021 uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri kwa baraza la CNC, pale alipokjutana na maafisa wa vyombo vya habari waliosimamishwa ili na kuiagiza CNC kuketi na viongozi wa vyombo vya habari vilivyochukuliwa vikwazo ili kuangalia kwa pamoja njia za kuondoa vikwazo hivyo.

Ilikuwa katika muktadha huu kwamba redio ya Bonesha FM, iliyoharibiwa baada ya mapinduzi yaliotibuka ya Mei 13, 2015, ilikubaliwa kuendelea na matangazo yake.

Kwa upande wa BBC, uamuzi wa kuondoa leseni ya uendeshaji nchini Burundi ulichukuliwa mnamo Machi 29, 2019 kufuatia ripoti ya vitendo vya mateso vinavyodaiwa kufanywa na maafisa wa kitaifa wa idara ya Ujasusi wilayani Kinindo wakati wa mzozo wa 2015. Ripoti ambayo ilipingwa vikali na serikali ya Burundi.

Gazeti la mtandaoni la Ikiriho liliidhinisha Jumatano hii, Juni 16 kuanza tena shughuli zake, lilikuwa limesimamishwa Oktoba 12, 2018 na Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri.

Alilikosoa gazeti hili kwa kusambaza, bila ushahidi, habari juu ya kesi ya utapeli wa pesa na tawi la Burundi la KCB (Benki ya Biashara ya Kenya). Aliwasilisha malalamiko ya kashfa.

CNC inatoa wito kwa wale wanaosimamia gazeti hili la mtandaoni "kuchukua hatua zote kuheshimu safu yake ya wahariri na sio kurudi kwenye makosa ambayo yalikuwa msingi wa kusimamishwa kwake".

Kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado viko chini ya vikwazo, CNC imesema, mazungumzo yataendelea na maafisa wao ili kufikia makubaliano.