KENYA

Kenya: Mwili wa polisi aliyekuwa akitafutwa wapatikana nyumbani kwa wazazi wake

Maofisa wa polisi wa Kenya wakiwa mbele ya Mahakama Kuu, huku mvua ikinyesha, Nairobi, Kenya, Novemba 14, 2017.
Maofisa wa polisi wa Kenya wakiwa mbele ya Mahakama Kuu, huku mvua ikinyesha, Nairobi, Kenya, Novemba 14, 2017. AP

Afisa wa polisi aliyehusishwa katika mauaji mbalimbali amekutwa amefariki dunia numbani kwao baada ya kutafutwa na idara za usalama kwa siku kadhaa. Msako huo ulimalizika hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo mwanamke wa miaka 34 anashukiwa kuwa aliwapiga risasi na kuwaua wanaume wawili mapema mwezi huu: afisa mwenzake wa polisi na mfanyabiashara ambaye alikuwa na uhusiano naye.

Mwili wa Caroline Kangogo, afisa wa polisi aliyetafutwa tangu Julai 5, ulipatikana mapema Ijumaa asubuhi nyumbani kwa wazazi wake. Alikuwa mafichoni kwa siku kumi. Timu ya polisi na vitengo maalum vya jeshi vilihamasishwa kumtafuta. Lakini bila mafanikio.

Caroline Kangogo anasemekana, hatimaye alijisalimisha usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa nyumbani kwa wazazi wake magharibi mwa Kenya, ambapo alikutwa amefariki dunia. Baada ya kusakwa kwa kipindi cha siku kumi na moja, mama yake ndiye ambaye alipata mwili wake siku ya Ijumaa asubuhi, mwendo wa saa mbili. Mwili wake ulionekana na jeraha la risasi kichwani na bunduki yake ikiwa karibu naye.

Mkurugenzi wa idara Jinai George Kinoti alitoa wito kwa umma kuwasaidia kumkamata polisi huyo ambaye alimtaja kuwa "Sugu, aliyejihami na hatari".

Kangogo amehudumu katika vituo mbali mbali vya polisi, pamoja na kitengo cha polisi wa Reli, kabla ya kupelekwa Nakuru, ambapo amekuwa akifanya kazi kwa karibu miaka mitatu.