RWANDA-USHIRIKIANO

Rwanda: Ufaransa yarejesha tena ubalozi wake nchini Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Elysee Jumatano Mei 23.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Elysee Jumatano Mei 23. Francois Mori/Pool via Reuters

Hatimaye Balozi mpya wa Ufaransa nchini Rwanda Antoine Anfre amewasilisha barua za utambulisho kwa kiongozi wa nchi hiyo Paul Kagame.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Ufaransa na Rwanda kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baada ya nchi hiyo kutokuwa na Balozi wa taifa hilo la Ufaransa kufuatia madai kuwa nchi hiyo ya bara Ulaya lilishiriki kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Hivi karibuni Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alifanya ziara nchini Rwanda,z iara iiliyoangaziwa kufungua ukurasa mpya wa historia ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

Bwana Macron ni rais wa pili wa Ufaransa kutembelea Rwanda baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 tangu rais wa zamani Nicolas Sarkozy alipotembelea taifa hilo mnamo 2010. Rwanda ilivunja uhusiano wake na Ufaransa mwaka 2006 kwa shutuma za mauaji ya kimbari.

Rais Macron alisema ziara yake nchini Rwanda itakuwa ya "sera ya ukumbusho, uchumi na kuangazia siku zijazo." Na kuongeza kwamba yeye pamoja na Rais Kagame walikubaliana ''kuanzisha ukurasa mpya wa mahusiano na kufanya miradi ya maendeleo.''