TANZANIA-UPINZANI

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania chaitisha maandamano

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama cha upinzani  CHADEMA nchini Tanzania
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA nchini Tanzania Tumaini Makene/ Chadema

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, kimeitisha maandamano ya amani kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wa chama hicho, Freeman Mbowe, aliyekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Mbowe anatarajiwa kufikishwa tena Mahakamani tarehe 5 mwezi Agosti jijini Dar es salaam kusikiliza kesi inayomkabili.

Mbowe alikamatwa siku 10 zilizopita mjini Mwanza na maafisa wengine wajuu wa chama chake saa chake kabla ya kuandaa kikao cha kushinikiza kufanyika kwa katiba mpya.

“Kumkamata Mbowe hakukuwa tu kumkamata yeye bali  ilikuwa ni ukiukwaji wa haki zetu” alisema Mnyika.

Chama hicho kimewataka wafuasi wake kujitokeza kwa wingi Mahakamani na kuandamana kwa amani kushinikiza kuachiliwa huru kwa Mbowe.

Mashtaka ya ugaidi hayana dhamana nchini Tanzania.