Barafu katika milima Kenya, Kilimanjaro na Rwenzori kuyeyuka
Imechapishwa:
Mamlaka ya dunia inayoshughulikia masuala ya hali ya hewa, katika ripoti yake ya mwezi Oktoba, imetahadharisha kuwa, kufikia mwaka 2040, barafu katika milima ya Kilimanjaro nchini Tanzania, Mlima Kenya na Rwenzori, itayeyuka kutokana na ongezeko la joto duniani. Nchini Uganda, watalaam kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori UWA wameanza kuchunguza hali ilivyo kwenye mlima Rwenzori, kila mwaka.
Carol Korir anaeleza zaidi, katika ripoti hii tuliyosaidiwa kuiandaa na mwandishi wa RFI Kifaransa jijini Kampala, Lucie Mouillaud .
Katika Ofisi yake, chini ya mlima Rwenzori, Nelson Enyagu, mtalaam wa wanayamapori na mtafiti , anaweka rekodi ya shughuli za kitalii zilizofanyika katika êneo la barafu, katika mlima huo, ripoti ya mwisho ikiwa ni mwezi Agosti.
Tulitembelea, maeneo mawili, ya Stanley na Margherita, kiwango cha joto kimepungua kwa kiasi kikubwa, katika hekari 0.26, tangu mara ya mwisho tulipofanya utafiti.
Kila baada ya miezi mitatu, watalaam hupanda mlima kwa siku 10 kwenda kuangalia hali ya barafu katika mlima huu.
Ni kazi kubwa ya kufanya kazi kwenye maeneo ya baridi kwa sababu ya hofu ya kutokea kwa magonjwa.
Hapa watalaam hawa wanasafisha vifaa wanavyotumia kufanya utafiti wao, kama anavyoeleza, Alfred Masereka.
Mkurugenzi wa utafiti Nelson Enyagu, anabaini kuwa kuna upungufu wa kiwango cha barafu.
Inakadiriwa kuwa kufikia mwaka 2025, hakutakuwa na barafu tena na uchunguzi unadhirihisha hilo.
Kwa sasa, kiwango cha barafu kwenye Mlima Rwenzori unakwenda umbali wa Kilomita 1.2. Tangu miaka ya 1960 eneo la Magharibi mwa Uganda, limeshuhudia kwa kiwango cha joto kwa sentigredi 0.5 kila baada ya miaka 20.
Kwa Zanzibar ni ishara nzuri sana kwa ushirikiano wa ufaransa na air france, kuwezekeza katika safari za ndege na kuunganisha kanda zetu, Afrika mashariki na ufaransa lakini kipekee, Zanzibara na Tanzania na Ufaransa.