Burundi: Marekani yaondoa vikwazo dhidi ya viongozi kadhaa

Rais Évariste Ndayishimiye, Agosti 2021 huko Bujumbura.
Rais Évariste Ndayishimiye, Agosti 2021 huko Bujumbura. REUTERS - EVRARD NGENDAKUMANA

Vikwazo hivyo vilianza kutumika mwaka 2015, katikati ya mzozo wa kisiasa wakati huo, uliotokana na kuwania kwa aliyekuwa rais wa zamani Nkurunziza kwa muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa kutetea uamuzi wake wa kuondoa vikwazo hivi, Marekani imebaini kuwa hali imearika baada ya kuchaguliwa kwa rais mpya Évariste Ndayishimiye mwaka mmoja nanusu uliopita. Agizo la Marekani la kufuta vikwazo hivi linaeleza kuwa hali ya mwaka 2015 iliyosabishwa na ghasia dhidi ya raia na ukandamizaji wa kisiasa "ilibadilishwa kwa kiasi kikubwa na matukio ya mwaka uliopita" nchini Burundi.

Marekani imetaja kukabidhiana madaraka baada ya uchaguzi wa mwaka 2020; kupungua kwa vurugu; na mageuzi yaliyoanzishwa na rais Évariste Ndayishimiye.

Watu 11 wanahusika na kuondolewa huku kwa vikwazo vya kifedha na mwisho wa marufuku ya kuingia nchini Marekani