Uganda

Kiongozi wa juu wa Jeshi la LRA akamatwa

Kiongozi wa Jeshi la Lord's Resistance Army, LRA
Kiongozi wa Jeshi la Lord's Resistance Army, LRA

Jeshi la Uganda limefanikiwa kumkamata Meja Caesar Acellam ambaye ni mmoja wa Kiongozi wa ngazi ya juu katika Kundi la Waasi la Lords resistancy army LRA linaloongozwa na Joseph Kony anayesakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.

Matangazo ya kibiashara

Meja Acellam amekamatwa akiwa nchini Afrika ya Kati na kisha akapelekwa nchini Sudan Kusini ambako ndiyo kuna makao makuu ya Kikosi kinachosaka Kundi la LRA ambalo limekuwa tishio kwa nchi kadhaa kwa sasa.
 

Kukamatwa kwa Meja Accellam kunatajwa kama mwanzo wa kuanguka kwa Kundi la LRA ambalo linatuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita pamoja na kuajiri watoto wadogo na alipotakiwa kuomba msahama alikataa.
 

Jeshi la Uganda linaliongoza jeshi la Umoja wa Afrika lililo na dhamana ya kuwakamata Viongozi wa LRA, baadhi yao wakiwa wanatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita mjini Hague nchini Uholanzi.
 

Miongoni mwa wanaowindwa na majeshi ni pamoja na Okot Odhiambo, Dominic Ongwen na Kony sambamba na Vincent Otti ambaye anadhaniwa kuwa ameshakufa.