Burundi-Sweden

Raia wa Burundi akamatwa nchini Sweden kwa tuhuma za kuendesha ujasusi

Bendera ya Burundi
Bendera ya Burundi

Polisi nchini Sweden imemtia nguvuni raia wa mmoja wa burundi kwa tuhuma za kuendesha vitendo vya ujasusi kwa raia wenzake wa burundi waliopewa hifadhi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mtu huyo raia wa burundi ambae hakutajwa jina lake, alikamatwa katika mji wa Oerebro ulio katikati mwa Sweden akituhumiwa kuendesha ujasusi kwa wakimbizi wa burundi walio pewa hifadhi nchini humo tangu mwaka 2010 na 2011.

Hakimu mkuu wa jiji la Oerebro Ronnie Jacobson amejizuia kumzungumzia mtu huyo, lakini amesema tu kwamba anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka arobani na zaidi.

Polisi wa Sweeden walimtia nguvuni raia huyo wa burundi tangu jumatatu na kumfikisha mahakama jana jumatano kujibu mashtaka yanayo mkabili ya ujasusi kinyume cha sheria, inayo chukuliwa kuwa kosa kubwa kwa sheria za nchi hiyo.

Kesi hiyo inatakiwa kuharakishwa kusikilizwa kabla ya tarehe 30 Mei mwaka huu, lakini hata hivyo hakimu mkuu wa mahakama hiyo amesema huenda muda ukaongezwa ili kufanya uchunguzi zaidi kuhusu mtuhumiwa huyo, na sababu za kuendesha ujasusi nchini humo kwa faida ya nchi nyingine, jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi hiyo.

Nchi za Sweeden na Norway zitowa hifadhi kwa wakimbizi wengi kutoka katika nchi za Afrika ya kati, hususan Burundi, Rwanda na Jamhuru ya Kidemokrasia ya Congo.