Kenya

Tusker FC ya Kenya kuweka kocha hadharani Ijumaa

RFI

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Kenya, Tusker FC wanatarajiwa kumtangaza kocha mpya wa klabun hiyo ya soka siku ya Ijumaa wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa klabu hiyo James Musyoki amebainisha kuwa makocha wengi wa kigeni waliomba kibarua cha kuinoa timu hiyo ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya kutupiwa virago kwa aliyekuwa kocha Sammy Pamzo Omollo Agosti 15 mwaka huu.

Amesema kuwa uongozi wa klabu hiyo utakutana Ijumaa na kuamua nani atapata nafasi ya kujaza hiyo na ambaye atakidhi viwango muhimu na kuwazidi wenzake.

Pamoja na kuingoza Tusker FC kupata ubingwa wa ligi Kuu ya Kenya kocha Omolo alifurushwa kutokana kufanya vibaya kwa timu hiyo kwenye mashindano ya Kombe la Kagame na kuenguliwa katika gatua za awali bila kushinda mechi hata moja.

Kwa sasa aliyekuwa kocha msaidizi wa Omolo, Bwana George Maina ndiye anashikilia nafasi hiyo kwa muda kabla ya kupatikana kwa kocha mpya siku ya Ijumaa.