Rwanda

Amnesty International yaituhumu Rwanda kwa ukiukwaji wa haki za binadamu

AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI

Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu duniani la Amnesty International kwa mara nyingine limetoa ripoti mpya iliyoiita “siri iliyojificha Rwanda”. 

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inaikosoa nchi hiyo kwa kuwatesa watuhumiwa wanaodaiwa kutaka kulipua mji wa kigali.

Shirika hilo limesema kuwa limekusanaya ushahidi wakutosha kuhusu kuteswa, kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwa watuhumiwa wanaoshikiliwa na maofisa usalama nchini humo.

Kwa upande wa serikali ya Rwanda kupitia kwa waziri wa Sheria Tarcisse Karugarama imekiri kutekelezwa kwa vitendo hivyo na iliomba radhi lakini si kitendo cha kiungwana kwa shirika hilo kurejea ripoti ambayo ilishafanyiwa utekelezaji.

Wakati huo huo watu watano wameuawa na zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya waasi kushambulia jimbo la Sudani kusini la Kordofani, tukio linaloelezwa kuwa nadra kutokea katika mji huo unaodhibitiwa na Serikali.

Msemaji wa Jeshi la Sudan, Sawarmi Khaled Saad, hajathibitisha idadi ya walioathirika na shambulizi hilo, huku Wapiganaji waasi wa kundi la Sudan People,s Liberation Movement-North wakikiri kufanya shambulizi hilo huku wakidai kuwa halikulenga Raia isipokuwa Jeshi, msemaji wa waasi hao Arnu Ngutulu ameeleza.

Mashambulizi ya mabomu hayo yametokea karibu na ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia watoto, UNICEF, shule na kituo cha polisi, Mratibu wa shughuli za misaada ya kibinaadam wa umoja wa Mataifa, AL-Za'tari ameeleza katika taarifa yake.