Uganda

Michuano ya CECAFA kufunguliwa rasmi kesho jijini Kampala Uganda

Kombe la CECAFA
Kombe la CECAFA RFI

Makala ya 36 ya mchezo wa soka ya CECAFA Tusker kuwania taji la timu bora Afrika Mashariki na Kati yataanza koshi Jumamosi jijini Kampala Uganda. 

Matangazo ya kibiashara

Tayari timu kumi na nne zitakazoshiriki katika kinyang'anyiro hicho zimewasili jijini Kampala Uganda,ikiwemo Sudan Kusini ambayo itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza na Malawi ambao wamealikwa kama wageni.

Mechi ya ufunguzi itachezwa kati ya watani wa jadi ambao pia ni wenyeji Uganda Cranes ambao ni mabingwa watetezi dhidi ya Harambee Stars ya Kenya katika uwanja wa Naambole mchunao ambao wapenzi wa soka katika mataifa hayo mawili wanauita Migingo Derby.

Ethiopia na Sudan Kusini pia watafungua mchuano wao hapo kesho.

Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayotou ni miongoni mwa wageni mashuhuri watakaoshuhudia mchuano huo wa ufunguzi.