SUDAN

Serikali ya Sudani yatangaza kuligawa jimbo la Kordofani Kusini

Makamu wa rais wa Sudan Ali Osman Taha
Makamu wa rais wa Sudan Ali Osman Taha sudaneseonline.org

Serikali ya Sudani imesema kuwa jimbo lenye mzozo la Kordofani Kusini litagawanywa na kutoa hadhi ya pekee kwa eneo la Magharibi ambalo linamilikiwa na watu wa jamii ya wafugaji wa kiarabu wa Miseriya. 

Matangazo ya kibiashara

Makamu wa rais Ali Osman Taha ametangaza kuanzishwa kwa jimbo la Kordofani Magharibi kama alivyokaririwa na shirika la habari la taifa SANA kwenye taarifa fupi ya habari.

Mchakato huo unaunda upya jimbo la Kordofani Magharibi ambalo liliondolewa mwaka 2005 kufuatia makubaliano ya amani baina ya Khartoum na jeshi la ukombozi la watu wa Sudani, ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 23.

Sudan na Sudani Kusini zimeshindwa kufikia makubaliano ya kutekeleza mapendekezo yaliyopitishwa mwezi Septemba ndani ya makataa ya hadi kufikia tarehe tano mwezi Disemba huku Umoja wa Afrika ukipendekeza kufanyika kwa kura ya maoni mwezi October mwaka ujao ili kujuanani anamiliki jimbo la Abyei.