KENYA

Wakenya wapiga kura huku mauaji ya polisi yakitia dosari zoezi hilo.

Wananchi wa Kenya wameendelea kusimama kwa muda mrefu kwenye mistari tangu alfajiri wakingoja kupiga kura zao katika uchaguzi mkuu wa kihistoria tangu kuzuka kwa ghasia zilizolikumba taifa hilo miaka mitano iliyopita, huku shambulizi la mapema dhidi ya polisi likiripotiwa kufanyika na kutia dosari zoezi hilo. 

mistari mirefu ya wapiga kura wakingoja kupiga kura zao
mistari mirefu ya wapiga kura wakingoja kupiga kura zao nation.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi unaonekana kuwa kipimo muhimu kwa ajili ya Kenya, huku viongozi wakiapa kuzuia kurejea kwa vurugu za umwagaji damu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-8 ambapo watu zaidi ya 1,100 waliuawa na waangalizi kurudia onyo la hatari ya kuanza upya kwa vita.

Wapiga kura wamesimama katika mistari kadhaa yenye umbali wa mamia ya mita wakiendelea kungoja kwa amani nje ya vituo vya kupigia kura kukamilisha zoezi hilo katika uchaguzi unaodaiwa kuwa na utata kuliko chaguzi zilizowahi kutokea nchini Kenya.
Mkuu wa tume ya uchaguzi na ukakuzi wa mipaka IEBC Ahmed Issack Hassan amesema kuwa wanatambua changamoto zilizojitokeza katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo na kuwataka wapigakura kuwawavumilivu.

Aidha Mvutano zaidi umetokea eneo la Pwani ikiwa ni pamoja na katika mji wa bandari wa Mombasa ambapo polisi sita waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti, ikiwa ni pamoja na shambulizi na vijana wapatao 200 wakiwa na silaha kama bunduki,pinde na mishale, saa kadhaa kabla ya ufunguzi wa vituo vya kupigia kura.