KENYA

Uhuru Kenyatta aendelea kuongoza matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Kenya

Zoezi la kuhesabu kura nchini Kenya linaendelea huku gombea urais kwa tiketi ya muungano wa Jubilee Uhuru Kenyatta akiendelea kuongoza katika matokeo ya awali na kufuatiw ana Raila Odinga wa muungano wa CORD.

Uhuru Kenyatta, mgombea urais wa muungano wa Jubilee
Uhuru Kenyatta, mgombea urais wa muungano wa Jubilee softkenya.com
Matangazo ya kibiashara

Tume huru ya uchaguzi na usimamizi wa mipaka IEBC imewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati zoezi hilo likiendelea hadi hapo matokeo rasmi yatakapo tangazwa juma moja baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura

Akizungumza mbele ya vyombo vya habari mwenyekiti wa tume hiyo Isaack Hassan amesema kuwa hakuna mgombea mwenye haki ya kujitangazia ushindi kwa matokeo haya ya awali kwa vile si matokeo rasmi.

Mgombea wa muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta anayeshitakiwa katika mahakama ya ICC kwa madai ya kuchochea vurugu za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008 hadi sasa anaongoza kwa asilimia 53.32% wakati Odinga akiwa na asilimia 42.29%