KENYA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ataja majina ya Mawaziri wanne kati ya 18

Rais wa Kenya Uhuru Mwigai Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Mwigai Kenyatta REUTERS/Presidential Press Service/Handout

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaja majina ya Mawaziri wanne kati ya 18 na kuwahakikishia wakenya kuwa atakuwa na Serikali ambayo itakuwa na kibarua cha kuiletea mabadiliko nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri walioteuliwa ni pamoja na Dr.Fred Okengo Matiang'i kuelekea kwenye wizara ya Habari, Mawasiliano na Tknolojia (ICT), Henry K. Rotich katika wizara ya Fedha , James Wainaina Macharia kulekea katika wizara ya Afya na Balozi Amina Mohamed Waziri katika wizara ya Mambo ya nje.
 

Wanne hawa watakuwa wa kwanza kuidhinishwa na Bunge la Nchi hiyo.
 

Kama ilivyokuwa ikitarajiwa na wengi Wanasiasa wengi wamekuwa wakitarajiwa kuteuliwa kwenye nafasi hizo, Rais Kenyatta amesema kuwa uteuzi wake umefuata matakwa ya kikatiba ya kutoa nafasi kwa wote lakini pia kwa kuzingatia uwezo wa Watu watakaokuwa na uwezo wa kuisaidia Kenya kupiga hatua ya maendeleo.
 

Rais Kenyatta amesema ametaja majina ya Viongozi hao wanne ili kulipa nafasi Bunge kuanza mchakato wa kutathimini na kuidhinisha majina hayo na kuahidi kutaja majina mengine siku chache zijazo.
 

Baadhi ya Wabunge wa Nchi hiyo wametoa wito kuwa Majina yatakayopelekwa Bungeni yasihusishe Majina ya Wanasiasa waliokataliwa na Wananchi.
 

Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto wako na Kibarua kigumu katika mchakato wa kuhakikisha kuwa wanawapatia Raia sura mpya katika Serikali ya Kenya kama walivyoahidi.