Burundi

Muswada wa sheria ya vyombo vya habari wazua mjadala mzito ndani ya Seneti Burundi

RFI

Muswada wa sheria unaohusu Wanahabari na Vyombo vya Habari ambao wanatakiwa kutaja vyanzo vya habari, umeendelea kuzua mjadala mkubwa nchini Burundi na kuwa gumzo kubnwa katika baraza la Seneta jijini Bujumbura nchini Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Maseneta kutoka chama cha Upinzani cha Uprona waliamua kuondoka mara moja ukumbini kwenye mjadala uliofuatia mara baada ya kukataliwa kupewa nafasi ya kuzungumza.
 

Katika Hatua Nyingine Jumuiya ya Wanahabari nchini Burundi imesema imefanikiwa kukusanya sahihi elfu kumi kutoka kwa wananchi kwa muda wa siku tano, kupinga muswada huo.
 

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Alexandre Niyungeko ametoa malalamiko yao kwa raisi wa taifa hilo na kumtaka asikibali kutangaza sheria hiyo ya waandishi wa habari.
 

Muswada huo unapingwa vikali na waandishi wa habari na mashirika ya kiraia kwa kuwa unalenga kukandamiza vyombo vya habari na waandishi wa habari.