TANZANIA

Takribani watu 30 wajeruhiwa kwa bomu nchini Tanzania

Takribani watu 30 wamejeruhiwa mjini Arusha nchini Tanzania baada ya mlipuko kutokea wakati wa ibada ya Jumapili ambayo ilihusu uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph mishale ya saa nne asubuhi. 

Waumini wakiwa nje ya kanisa jipya la Mt. Joseph kabla ya mlipuko
Waumini wakiwa nje ya kanisa jipya la Mt. Joseph kabla ya mlipuko jumamtanda.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa kanisa aliyejulikana kama Padri EustatTarimo ameongea na rfikiswahili na kuelezea tukio hilo lilitokea ghafla na kusambaratisha waumini na viongozi waliokusanyika kuabudu katika eneo hilo.

Padre Tarimo ameeleza kuwa watu takribani 30 wamejeruhiwa kutokana na tukio hilo ambapo waumini walishirikiana kuwapakia kwenye magari kwa ajili ya kuwafikisha hospitali.

Hadi sasa haijajulikana chanzo cha tukio hilo ambalo limesababisha kuvurugika kwa ratiba ya ziara ya kichungaji ya Balozi wa Papa nchini Tanzania.