KENYA

Bunge la Kenya laidhinisha majina 16 ya mawaziri

Bunge la Kenya
Bunge la Kenya kiongozi.co.ke

Bunge nchini Kenya limeidhinisha majina kumi na sita ya wateule wa nafasi ya uwaziri walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto na wanatarajiwa kuapishwa baadaye leo kuanza majukumu ya kutumikia Baraza la Mawaziri. 

Matangazo ya kibiashara

Awali kabla ya kuidhinishwa kwa majina hayo ulizuka mjadala mkali kuhusu kuachwa nje kwa Bi Phyilis Kosgey Kandie ambaye aliteuliwa na rais Kenyatta kuwa waziri wa Afrika Mashariki ,Utalii na Biashara kwa kile ambacho kamati ya bunge kuhusu uteuzi kudai kuwa alishindwa kujieleza mbele ya tume hiyo wakati wa mahojiano.

Hata hivyo bunge halikuridhishwa na sababu hizo hatua ambayo ilimfanya mwakilishi wa wanawake bungeni wa Kaunti ya Nairobi Rahel Alshabeshi kuwasilisha mswada wa kuifanyia marekebisho ripoti hiyo na kumwidhinisha bi Kandie.

Baada ya kufanyiwa marekebisho kwa ripoti hiyo majina kumi na sita yaliidhinishwa ikiwa ni pamoja na la waziri Kandie ambapo wanataraji kuapishwa na rais leo Jumatano kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yao.