Jeshi la polisi Kenya lakanusha kukithiri kwa uhalifu nchini humo
Jeshi la polisi nchini Kenya limekanusha madai kuwa wameshindwa kudhibiti hali ya usalama katika taifa hilo, haswa baada ya kutokea kwa visa vya utovu wa usalama katika kaunti za Bungoma na Mandera siku kadhaa zilizopita.
Imechapishwa:
Inspekta wa polisi generali David Mole Kimayo kupitia kwa msemaji wake Masoud Mwinyi amesema kuwa hadi sasa bunduki kumi aina ya AK 47 na silaha nyingine na risasi 463 tayari zimesalimishwa kwa maafisa wa usalama katika kaunti ya Mandera.
Aidha katika Kaunti ya Bungoma Magharibi mwa Kenya, afisa huyo amesema kuwa watu 328 wametiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani kufuatia matukio ya uhalifu yaliyotokea huko Bungoma na Teso na amewataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kusalimisha silaha kwa hiari.
Pia Kimayo amekanusha taarifa za vyombo vya habari kuwa matukio ya uhalifu yamekithiri nchini humo nakusema kuwa hadi sasa matukio hayo yamedhibitiwa hasa maeneo ya Garisa na kwamba wanayaangazia matukio ya uhalifu ya huko Mandera.