UGANDA

Mkutano wa Jumuiya ya Madola waazimia kumaliza umasikini kwa nchi wanachama

Mkutano wa saba wa Jumuiya ya Madola unaoendelea huko kampala nchini Uganda umeazimia kufanya kila linalowezekana kumaliza umasikini kwa mataifa wanachama. 

Wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Madola
Wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Madola vivalanka.com
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia wajumbe wanaohudhuria mkutano huo rais wa Sri Lanka Rajapaska Mahinda ambaye nchi yake imeshuhudia mabadiliko makubwa ya uchumi kutokana na utawala wa ugatuzi wa mamlaka, amewahimiza viongozi wote wanaohudhuria mkutano huo kutumia mbinu zote kuhakikisha umasikini unamalizika.

Mkutano huo umewakutanisha viongozi wa serikali za mitaa kutoka nchi wanachama wa jumuiya za madola ili kujadili namna ya kukuza uchumi bila kutegemea serikali kuu.

Mkutano huo ambao unamalizika kesho unatarajia kutoa maazimio ambayo yatatumika kama dira ya kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea kuhusu kugatua madaraka kwenda kwa wananchi zaidi na kukuza uchumi.