Waziri wa zamani wa Kenya ateuliwa kuongoza taasisi ya biashara ya umoja wa mataifa
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amemteua waziri wa zamani wa Kenya na mbunge Mukhisa Kituyi kuongoza taasisi ya biashara na maendeleo ya umoja huo UNCTAD wakati mkuu wa taasisi hiyo atakapoachia madaraka mwishoni mwa mwezi wa nane.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Moon amemteua Mukhisa kuongoza taasisi hiyo kwa muhula wa miaka minne utakao anza Septemba 1 mwaka 2013 taarifa ya umoja huo imeeleza na kuongeza kuwa kuteuliwa kwake lazima kuthibitishwe na mkutano mkuu wa Umoja huo.
Endapo atathibitishwa kitui atachukua nafasi ya Supachai Panitchpakdi wa Thailand ambaye ametumikia taasisi hiyo ya umoja wa mataifa kwa mihula miwili tangu alipochukua nafasi hiyo Septemba Mosi mwaka 2005.
Kituyi alikuwa mbunge wa bunge la Kenya kwa miaka 15 tangu mwaka 1992 na amelitumikia taifa la Kenya kama waziri wa biashara na viwanda kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2007.