Afrika Ya Mashariki

Maisha ya watu wa Gulu, Uganda na mabadiliko yake baada ya vita

Sauti 09:29

Uganda ni miongoni mwa nchi ambazo zimepitia mazingira ya vita kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi. Ukiangalia vita vya ndani Uganda ilikabiliana vikali na waasi wa LRA wakiongozwa na Joseph Kony. Baada ya vita hivyo, maisha ya wananchi wa Uganda yalibadilika. Katika Makala ya Afrika Mashariki leo hii tunaangazia maisha mapya ya wananchi wa huko Gulu, Uganda.