KENYA-MASHAMBULIZI

Watu wanne wauawa katika shambulio huko Garisa nchini Kenya

Mji wa Garisa
Mji wa Garisa

Takriban watu wanne wameuawa akiwemo polisi mmoja jana jioni katika shambulio linalo kisiwa kuendeshwa na waasi wa kundi la wapiganaji wa kiislam la nchini Somalia la Al Shabab dhidi ya kituo kimoja cha polisi katika mji wa Garisa nchini Kenya

Matangazo ya kibiashara

Duru za polisi na za shirika la msalaba mwekundu nchini humo zimethibitisha kutokea kwa shambulio hilo katika mji wa Garisa lililoendeshwa na wapiganaji wa Al shabab waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito na kushambulia kituo cha polisi cha Galmagala ambapo Mutea Irigo kiongozi mmoja kati ya viongozi wa juu katika wizara ya mambo ya ndani amesema askari polisi mmoja amepoteza maisha katika tukio hilo.

Eneo hilo la tukio lipo kwenye umbali wa kilometa zaidi ya hamsini na mpaka na Somalia. Ma mia kadhaa ya watu wametoroka makwao kufuatia hofu ya kutokea tena kwa shambulio jingine kama hilo.

Hakuna kundi lolote ambalo limekwisha jigamba kuhusika na shambulio hilo.

Eneo la Kenya lenye umbali wa kilometa mia saba mpakani na Somalia hususan katika eneo la Mandera, Wajir, Garisa, limekuwa likishambuliwa ambapo mashambulizi mengi yamekuwa yakilenga vituo vya polisi, ma hoteli na migahawa.

Viongozi wa Kenya wamesema bila shaka shambulio hilo limetekelezwa na wapiganaii wa kundi la Al Shabab linalo pambana na serikali ya kenya tangu Octoba mwaka 2011 Kusini mwa Somalia

Mwezi Mei askari polisi mmoja aliuawa katika shambulio kama hilo dhidi ya kituo cha Polisi katika mji wa mandera, huku watu wengine kumi wakiuawa katika mashambulio mawili tofauti kwenye hoteli jijini Garissa mwezi Januari na Aprili.