TANZANIA-RWANDA

Maoni ya watanzania waishio nchini Rwanda kuhusu hatuwa ya serikali yao kuwafukuza Wanyarwanda waishio nchini Tanzania kinyume cha Sheria

Eneo la Rusomo mpakani mwa Rwanda na Tanzania
Eneo la Rusomo mpakani mwa Rwanda na Tanzania

Zaidi ya wanyarwanda elfu sita wamepokelewa nchini Rwanda wakitokea nchini Tanzania. Raia hao waliokuwa wanaishi nchini Tanzania kinyume cha sheria, na sasa serikali ya Rwanda imewapa hifadhi ya muda katika kambi iliyopo kilometa 6 kutoka mpaka wa Rwanda na Tanzania.Muandishi wetu wa huko Kigali nchini Rwanda Bryson Bichwa amezungumza na baadhi ya raia wa Tanzania waishio nchini Rwanda, kutaka kujua maoni yao juu ya hatua ya serikali ya Tanzania na maisha yao kwa ujumla nchini Rwanda.