Habari RFI-Ki

Wabunge Kenya kujadili hatima ya kesi z ICC dhidi ya Kenyatta na Ruto

Sauti 08:55
RFI

Mahakama kuu jijini Nairobi inatarajiwa kutoa mwelekeo hii leo kuhusu kesi iliyowasilishwa na shirika moja lisilo la kiserikali ya kuitaka mahakama kuwazuia Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kuhudhuria kesi za uhalifu dhidi ya binadamu zinazowakabili wawili hao pamoja na mwanahabari Joshua Sang katika mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICC. Makala ya Habari Rafiki leo hii inaangazia sakata hilo linaloendelea nchini Kenya.