Gurudumu la Uchumi

Katiba mpya Tanzania na nafasi yake katika ukuaji wa uchumi

Sauti 09:40

Katiba ya nchi ni mhimili muhimu katika kutoa dira ya maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Tanzania ni moja ya nchi ambazo ziko katika mchakato wa kusaka katiba mpya. Leo makala ya Gurudumu la Uchumi  itaendelea  kuangazia namna katiba mpya inaweza kusaidia ukuaji wa uchumi.