SUDANI KUSINI - IGAD

Jumuiya ya nchi za Igad kuwatuma wanajeshi wake nchini Sudani Kusini kulinda amani.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed hiiraan.com

Uongozi wa Jumuiya ya maendeleo ya mataifa ya Igad, inayo jumuiya nchi saba za ukanda wa Afrika mashariki, umekubaliana kuvituma vikosi nchini Sudani Kusini ambako machafuko yanaendelea kuchacha tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed amesema Igad imeidhinisha azimio la kutuma wanajeshi 5.500, wakati nchi nyingine zikiendelea kutafakari kuhusu hatuwa hiyo.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Kenya Kikosi hicho kitakuwa na jukumu la kulinda usitishwaji mapigano unatarajiwa kufikiw akatika siku za usoni baina ya waasi na wanajeshi wa serikali ya Juba. Hata hivyo hakuweka bayana, ni lini kikosi hicho kitatumwa huko Sudani Kusini.

Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ys Igad ambao ulitarajiwa kufanyika alhamisi juma hili mjini Juba umeahirishwa, ambapo serikali ya Juba imsema hatuwa hiyo imechukuliuwa baada ya ukaribu wa kikao cha Umoja wa Afrika kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa januari na ambao utajadili kuhusu mzozo wa Sudani Kusini.

Hayo yanajiri wakati wajumbe wa serikali ya rais Salva Kiir na wale wa Riek Mashar wakiendelea kulumbana katika mazungumzo ya kufikia usitishwa mapigano jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Waasi wanaongozwa na Riek Mashar aliyewahi kuwa makam wa rais nchini Sudani Kusini kabla ya kutumuliwa na rais Salva Kiir wanataka serikali ya Juba kuwaacha huru wajumbe 11 wanaozuiliwa na serikali, kabla ya waokuendelea na mazungumzo na kusaini mkataba wa kusitisha mapigano, jambo ambalo serikali ya Juba imeendelea kulipinga.