Habari RFI-Ki

Hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kwenda ICC

Sauti 10:15

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekabidhi madaraka kwa naibu wakeWilliam Ruto, kukaimu urais nchini humo wakati atakapokuwa katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi kesho Jumatano kuhudhuria kikao kuhusu kesi inayomkabili ya kuchochea na kufadhili machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007. Kenyatta amekubali kuhudhuria kikao hicho, kama mtu binafasi wala siorais wa Kenya.Kipindi cha Habari Rafiki kitazungumzia vipi hatua hiyo ya rais Kenyatta kukabidhi madaraka na kuhudhuria kikao kuhusu kesi yake