KENYA-TANZANIA

Ndege za KQ kuanza safari kamili nchini Tanzania baada ya Uhuru na Kikwete kutatua mzozo

Ma rais Kikwete wa Tanzania na Uhuru wa Kenya
Ma rais Kikwete wa Tanzania na Uhuru wa Kenya

Siku chache baada ya Serikali ya Tanzania kutangaza kupunguza safari za shirika la ndege la Kenya kutoka safari 42 hadi 14, viongozi wa nchi hizo mbili wamekutana nchini Namibia na kukubaliana kutatua mzozo huu.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Tanzania kusitisha safari za ndege za shirika la Kenya, imekuja baada ya utawala wa Kenya kuzuia mabasi ya Tanzania yanayobeba watalii kufika kwenye uwanja wake wa ndege wa Jomo Kenyatta hali iliyozua utata kuhusu uhusiano wa nchi hizi mbili.

Kando na sherehe za kuapishwa kwa rais wa Namibia, rais wa Kenya, Uhuru Mwigaye Kenyatta na mwezake wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete walifanya mazungumzo yaliyodumu kwa takribani dakika 45 na kukubaliana kimsingi kuondoa utata uliopo baina ya mataifa haya mawili kuhusu swala hilo.

Akiziungumza hapo jana muda baada ya kureja nchii Kenya waziri wa mambo ya nje Amina Mohammed amewambia waandishi wa habari kwamba safari za shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways litarudi kufanya safari zake mara 42 kwa wiki kama ilivyokuw ahapo awali, huku huku ma basi ya usafiri kutoka Tanzania yataruhusiwa kufika hadi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta (JKIA) baada ya mazungumzo ya ma rais wa nchi hizi mbili.

Waziri huyo ameemdelea kuwa Viongozi hao wawili walikubaliana kurejeshwa kwa hali kama ilivyo.

Pia ilikubaliwa kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa Kenya na Tanzania , mawaziri wa Utalii na Usafiri watakutana jijini Dar es Salaam katika mkutano utaohudhuriwa opia na marais Kenyatta na kikwete kujaribu kutafuta kwa pamoja ufumbuzi wa malalamiko ambayo yamesababisha kupunguzwa kwa safari za ndege za Kenya kwenda Tanzania na ile ya kuzuia ma basi ya watalii kufika kwenye uwanaj wa ndege wa Kenya.

Ma rais Kenyatta na Kikwete wamesisitza haja ya kuendelea kujadili kwa uwazi masuala yanayoathiri undugu na uhusiano wa muda mrefu baina ya mataifa haya mawili.

Kumekuwa na maswali mengi tu ya kujiuliza iwapo swala hili limezua mzozo baina ya  Tanzania na Kenya. waziri wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohamed yeye anaona kwamba ni jambo la kawaida kwani hata ndugu wawili wawili hugombana na kupatana.

Kwa mujibu wa makubaliano haya, sasa magari ya kubeba watalii kutoka Tanzania yataruhusiwa kufika uwanja wa ndege wa kimataifa Jomo Kenyatta kuchukua watalii, huku safari za shirika la ndege la Kenya, KQ zikirejea kuwa 42 kama ilivyokuwa hapo awali.