Kenya-Ugaidi

Siku ya pili ya maombolezo, vilio vyaongezeka baada ya familia kuwatambua ndugu zao

Wakenya wakiendelea kutowa damu
Wakenya wakiendelea kutowa damu

Leo Jumatatu ikiwa siku ni siku ya pili ya maombolezo huko Kenya, baada ya kutokea mauaji ya wanafunzi mia-moja-arobaini-na-nane waliouawa na magaidi wa Al Shabab, wanafunzi walionusurika wameeleza masaibu yao wakati huu jamii zilizopoteza wapendwa wao zikiendelea kuangua vilio baada ya kutambua miili ya waliouawa.

Matangazo ya kibiashara

Wingu la huzuni limeendelea kutanda kote nchini Kenya, hasa katika jiji la Nairobi ambapo zoezi la kuhuzunisha la kutambua wanafunzi waliouawa na magaidi ya Al Shabab likiendelea.

wanafunzi walionusurika wameendelea kutowa ushuhuda wao kuhusu tukio hilo na mbinu walizotumia ili kunusurika, ambapo mmoja ameeleza kwamba alijificha kwenye uvungu wa kitanda na ambaye anashukuru Mungu kwa kunusurika kifo.

Wakati wa shambulio hilo wasichana wawili walijitosa chooni na kujifungia humo wakati risasi zilipokuwa zikifyatuliwa na ndipo kunusurika.

hali ya huzuni imeendelea kutanda nchini Kenya, kila mmoja akiendelea kumkumbuka ndugu yake aliepoteza maisha katika shambulio hilo, akiwemo baba wa askari polisi mmoja alipoteza maisha katika shambulio hilo ambae imekuwa vigumu kuelewa kilichotokea.

Mama mmoja aliempoteza mumewe katika shambulio hilo amesema kuishiwa na nguvu huku akibubujikwa na machozi kila wakati.

Hii leo Jumatatu wananchi wa Kenya wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi hapa Nairobi kuweza kutoa damu ya kusaidia majeruhi ambao bado wanatibiwa katika mahospitali tofauti.

Hapo jana kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ametowa wito wa kuwaombea wale wote walipoteza maisha katika shambulio hilo la kaskazini mashariki mwa Kenya karibu na Somalia.

kiongozi huyo amesema sala na maombi ya pamoja iwaendee wale wote walipoteza maisha katika shambulio hilo na matrka wote waliotekwa katika maeneo mbalimbali ya dunia.