Wazanzibar wajiandaa kupiga kura kesho Jumapili, wanaharakati kukamatwa mjini Goma nchini DRC.

Sauti 21:13

Katika makala hii ya mtazamo wako kwa yaliyojiri wiki hii tumeangazia mchakato wa uchaguzi wa marudio unaopangwa kufanyika hapo kesho siku ya jumapili marchi 20 ambapo hali ya kisiasa inadhirisha kuwepo na mgawanyiko katika baadhi ya vyama vya upinzani baada ya chama cha wananchi CUF kuelezea kuwa hakitashiriki kwenye uchaguzi huo.Maandamano ya wanaharakati wa kutetea demokrasia na utawala bora nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Ufaransa kuendelea na azma yake ya kutekeleza mapambano yake dhidi ya makundi ya kigaidi baada ya mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya watu kadhaa kwenye eneo la ufukweni la grand bassam, nchini Cote d'Ivoire;Lakini pia kimataifa tumeangazia mkutano wa umoja wa ulaya kuhusu wakimbizi wanaoingia uturuki.Ungana nami Reuben Lukumbuka katika makala hii.