Burundi yaishtumu Rwanda kuipangia mauaji ya kimbari

Sauti 16:00

Chama tawala nchini Burundi kinamshtumu rais wa Rwanda Paul Kagame kwa kupanga mauaji ya kimbari nchini mwake. Bujumbura imekuwa ikiishtumu Kigali kuwapa mafunzo ya kijeshi wakimbizi waliokimbilia nchini humo ili kuishambulia serikali ya rais Piere Nkurunziza. Madai haya yamekanushwa vikali na serikali ya Rwanda.