UGANDA-UANAHABARI

Cheti cha Digri chatakiwa kwa kuripoti vikao vya Bunge

Aslari polisi wa Uganda mjini Kampala, Machi 2016.
Aslari polisi wa Uganda mjini Kampala, Machi 2016. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI

Uongozi wa Bunge nchini Uganda unasema hautawaruhusu waandishi wa Habari wasio na cheti cha Digrii katika maswala ya Uanahabari kuripoti vikao vya Bunge.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa Mawasialino katika Bunge hilo lenye makao yake jijini Kampala, Chris Obore, amesema hatua hii imechukuliwa ili kuhakikisha kuwa wanahabari waliofuzu ndio wanaoruhusiwa bungeni lakini pia wale ambao wamekuwa wakiripoti katika majengo ya bunge kwa zaidi ya miaka mitano hawataruhusiwa kuendelea na kazi hiyo.

Aidha, Bwana Obore amedai kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia taaluma hii kuomba fedha za nauli kutoka kwa wabunge na kujifanya kuwa wanahabari.

Hata hivyo, hatua hii imekashifiwa na baadhi ya wanahabari ambao hawana cheti cha Digrii kwa kile wanachosema ni uonevu.