RWANDA-MAAFA

Watu zaidi ya hamsini wapoteza maisha Rwanda

Wilaya ya Rubavu,  Rwanda, moja ya wilaya zilizoathirika zaidi na mvua zilizonyesha mwishoni mwa juma lililopita.
Wilaya ya Rubavu, Rwanda, moja ya wilaya zilizoathirika zaidi na mvua zilizonyesha mwishoni mwa juma lililopita. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI

Watu wasiopungua hamsini wamepoteza maisha mwishoni mwa wiki hii iliyopita katika wilaya nne za vijijini nchini Rwanda kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha, vyanzo rasmi vimebaini Jumatatu hii.

Matangazo ya kibiashara

"Usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Mei 8, 2016, mvua kubwa zilisababisha maporomoko ya ardhi katika sehemu mbalimbali za Rwanda na kusababisha watu wengi kupoteza maisha na mali nyingi kuteketea". Serikali ya Rwanda imesema katika taarifa kwamba imeorodhesha vifo vya watu arobaini na tisa.

Wilaya zilizoathirika zaidi ni Gakenke, kaskazini mwa nchi, ambapo watu 34 walipoteza maisha. Wilaya nyingine ni zile za Muhanga, Rubavu na Ngororero, magharibi mwa Rwanda.

Nchini kote mwishoni mwa wiki iliyopita , "nyumba zaidi ya 500 zilipelekwa na mafuriko na sehemu mbalimbali za barabara zimeharibika," imesema taarifa hiyo.

Rwanda, nchi ndogo na yenye watu wakazi wengi, inakabiliwa na mmomonyoko wa ardhi na maporomoko ya udongo. Lakini mwaka huu, msimu wa mvua umesababisha vifo vingi.

Kati ya Januari na Aprili, takriban watu 67 walipoteza maisha nchini kote, kwa mujibu wa Wizara ya Rwanda yende dhamana ya Usimamizi wa Majanga, ikiwa ni pamoja watu 12 kwa muda wa siku katika viunga vya mji mkuu Kigali.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Rwanda iliweza kupunguza idadi ya ajali ya aina hii, kutokana hasa na sera ya kuhamishwa kwawatu wanaoishi katika maeneo hatari.

Lakini mwaka huu, ajali nzimeongezeka, mamlaka imesema hali ya mabadiliko ya hewa (El Niño) ndio husababisha hali hii.