KENYA-WAKIMBIZI
Kenya yajianda kuzifunga kambi za Daadab na Kakuma
Imechapishwa:
Kenya imetangaza kuwa itatumia Dola Milioni 10 kufunga kambi kubwa ya wakimbizi duniani ya Daadad na ile ya Kakuma.
Matangazo ya kibiashara
Waziri wa Mambo ya ndani Joseph Ole Nkaissery amesema hatau hii inachukuliwa kwa sababu za kiusalama.
Serikali ya Kenya imekuwa ikisema kuwa kambi hiyo ya Daada inayowapa hifadhi wakimbi raia wa Somalia zaidi ya Lakini Tatu, imekuwa ikitumiwa kama maeneo ya kuwapa hifadhi magaidi wa Al Shabab.
Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya kibinadamu yametoa wito kwa Kenya kufikiria tena uamuzi huo kwa hofu kuwa wakimbizi hao huenda wakashambuliwa na Al Shabab ikiwa watarudi Somalia.