UGANDA-MUSEVENI

Museveni aapishwa Kampala

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. RFI

Maelfu ya raia wa Uganda, wakiwemo viongozi kadhaa wa bara la Afrika wameshuhudia kuapiashwa kwa rais Yoweri Kaguta Museveni kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Akiwahotubia maelfu ya raia wa Uganda na wageni wengine mashuhuri katika uwanja wa Kololo jijini Kampala, Rais Museveni amesema, katika uongozi wake wa miaka mitano ijayo, atahakikisha kuwa Uganda inakuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.

Kuhusu usalama, rais Museveni amesema nchi yake kwa muda wa miaka 30 alizokuwa madarakani ina amani ya kutosha ndnai ya miaka 500 ya historia ya nchi hiyo, na kutoa wito kwa mataifa ya Afrika kusaidia nchi zingine kupata amani kama hiyo.

Museveni alitumia sherehe za leo pia kuishtumu Mahakama ya Kimataifa ya ICC, ambayo imeelezea kuwa taasisi ambayo haina maana.

Alitoa kauli hiyo wakati akimtambulisha rais wa Sudan Omar Al Bashir anayetafutwa na Mahakama ya ICC, kwa sababu ya mauaji ya maelfu ya watu katika jimbo la Darfur.

Pamoja na hotuba ya rais Museveni, wananchi wa Uganda waliofika katika sherehe hiyo waliburudishwa na bendi ya wanajeshi.

Lakini pia ndege za kivita zilipaa angani kuonesha ushupavu wa jedhi la UPDF.

Sherehe zingine kama hizi zitafanyika baada ya uchaguzi wa mwaka 2021. Je, rais Museveni mwenye umri wa miaka 71 atawania tena ?