UGANDA-BESIGYE

Kizza Besigye aendelea kusalia gerezani

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amehamishiwa katika Gereza ya Luzira jijini Kampala kutoka Moroto alikokuwa anazuiliwa.

Kizza Besigye mbele ya vyombo vya habari Kampala, Februari 13, 2016 kabla hajafungwa.
Kizza Besigye mbele ya vyombo vya habari Kampala, Februari 13, 2016 kabla hajafungwa. Isaac Kasamani / AFP
Matangazo ya kibiashara

Besigye amefunguliwa mashtaka ya uhaini baada ya kujiapishwa kama rais wa Uganda siku ya Alhamisi juma lijalo.

Serikali ya Uganda inasema imemhamisha Besigye katika Gereza la Luzira kwa sababu za kiusalama lakini pia wamezingatia kuwa alikuwa mgombea urais.

Chama chake cha FDC na wanaharakati wa haki za binadamu wamekashifu kuzuiliwa kwa Besigye na kufunguliwa kwa mashtaka hayo.

Aliyekuwa Waziri Mkuu Amama Mbabazi ambaye pia aliwania urais, amesema anajitolea kuwa Wakili wa Besigye.