UGANDA-BESIGYE

Besigye kufikishwa mahakamani kwa kosa la uhaini

Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye.
Kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye. REUTERS/Thomas Mukoya

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne hii, baada ya kutuhumiwa kosa la uhaini.

Matangazo ya kibiashara

Besigye anakabiliwa na tuhuma za kujitangaza kuwa mshindi wa rais wa Uganda mwezi February jwakati ambapo Rais Yoweri Museveni ndiye alitangazwa mshindi na mahakama ya juu nchini humo. Wiki iliyopita Museveni aliapishwa kuwa Rais wa Uganda.

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, hivi karibuni alihamishiwa katika Gereza ya Luzira jijini Kampala kutoka Moroto alikokuwa anazuiliwa.

Serikali ya Uganda inasema ilimhamisha Besigye katika Gereza la Luzira kwa sababu za kiusalama lakini pia wamezingatia kuwa alikuwa mgombea urais.

Chama chake cha FDC na wanaharakati wa haki za binadamu wamekashifu kuzuiliwa kwa Besigye na kufunguliwa kwa mashtaka hayo.

Aliyekuwa Waziri Mkuu Amama Mbabazi ambaye pia aliyewania urais, hivi karibuni alisikika akisema kuwa anajitolea kuwa Wakili wa Besigye.