BURUNDI-RWANDA-DIPLOMASIA

Burundi yaituhumu kwa mara nyingine Rwanda

Serikali ya Bujumbura imeendelea kuinyoohea kidole cha lawama nchi jirani ya Rwanda kuwa chanzo cha mgogoro nchini mwake.
Serikali ya Bujumbura imeendelea kuinyoohea kidole cha lawama nchi jirani ya Rwanda kuwa chanzo cha mgogoro nchini mwake. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama

Serikali ya Burundi imeituhumu Rwanda kwa mara nyingine tena kuwa na lengo la kuhatarisha usalama wake. Kwa sasa serikali ya Burundi imetoa ripoti kamili juu ya suala hilo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti yenye kurasa ishirini na tano inaonyesha jinsi Rwanda imekua ikiingilia katika masuala ya Burundi na makundi ya waasikwa kuzorotesha utawala wa Pierre Nkurunziza.

Ripoti hiyo ambayo imetolewa mwaka mmoja baada ya jaribio la mapinduzi la mwezi Mei 2015, inaanza kwa kukumbusha yale yaliyotokea miaka ya nyuma. Historia inaanza na mwaka 1959. Mwaka huo, maelfu ya Wanyarwanda walikimbilia Burundi baada ya mauaji katika nchi yao. Ripoti hiyo inazungumzia "maeneo yaliyovamiwa" na wakimbizi wa Rwanda kutoka jamii ya Watutsi mjini Bujumbura. Na kuhakikisha kwamba maeneo hayo ni yale leo yamekua ni kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Rais Nkurunziza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, imekua tu kama kisingizio, kwa maandamano yaliyotajwa na utawala wa Pierre Nkurunziza kuwa na lengo la kuanzisha "uasi". Ripoti hii inahakikisha kwamba machafuko yalianza kabla ya kampeni za uchaguzi mwaka jana. Kulikua na mashambulizi yaliokua yakiendeshwa na makundi ya waasi, mashambulizi ambayo yalikua yakidhaminiwa na Rwanda.

Kwa nini? Kwa sababu utawala way Kagame unajihisi kuwa vibaya kutokana na mchakato wa maridhiano nchini Burundi pamoja na mfumo wa kisiasa, unaoendeswa kulingana na ibdadi inayohitajika kikabila. Haya ni mafanikio makubwa kwa Burundi, kwa mujibu wa ripoti hii, wakati nchini Rwanda, hakujakua na mjadalawowote. Kwa mujibu serikali ya Bujumbura, utawala wa Kigali umepata uhalali wakekutokana na hali iliyotokea Rwanda miaka ya nyuma. Ni kutokana na hali hiyo, ripoti hiyo inahitimisha, Rwanda inataka kuhatarisha usalam wa jirani yake.

Itafahamika kwamba si mara ya kwanza Burundi kuishambulia kimaneno na kuituhumu Rwanda kutaka kuzorotesha usalama wake. Hata hivyo Rwanda imekua ikikanusha tuhuma dhidi yake na kusema haitishwi na kauli mbovu za mara kwa mara za serikali ya Burundi.