BURUDI-MAZUNGUMZO

Serikali ya Burundi kushiriki mazungumzo

Askari polisi wakirusha mabomu ya machozi wakati wa maandamano mjini Bujumbura Mei 21, 2015.
Askari polisi wakirusha mabomu ya machozi wakati wa maandamano mjini Bujumbura Mei 21, 2015. REUTERS/Goran Tomasevic/Files

Serikali ya Burundi imethibitisha kushiriki katika mazungumzo ya amani, yanayoongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yameratibiwa kufanyika kati ya tarehe 21 na 24 mwezi huu katika Makao makuu ya Jumuiya hiyo mjini Arusha nchini Tanzania.

Mshauri mkuu wa rais katika masuala ya Mawasiliano, Willy Nyamitwe amesema wamepokea mwaliko na watashriki katika mazungumzo hayo.

Hata hivyo, muungano wa vyama vya upinzani CNARED unasema hautashiriki katika mazungumzo hayo kwa sababu haujapokea mwaliko kitoka kwa mratibu wa mazungumzo hayo, rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa.