UGANDA-USALAMA

Watu 29 watekwa nyara Uganda

Watu wasiofahamika wakiwa wamejihami kwa silaha wamewateka watu 29 katika Wilaya ya Yumbe nchini Uganda, karibu na mpaka wa Sudan Kusini.

Askari poli wa Uganda akipiga doria katika moja ya mtaa wa Kampala, Machi 2015.
Askari poli wa Uganda akipiga doria katika moja ya mtaa wa Kampala, Machi 2015. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa utekaji nyara huo ulifanyika mapema wiki hii.

Mwenyekiti wa Wilaya hiyo Taban Yasiin anasema kuwa watu hao huenda wamepelekwa nchini Sudan Kusini.

Kabla ya utekeaji nyara huo, kundi hilo la watu lilivamia wilaya nyingine ya Moyo na kuiba mifugo na vyakula kutoka kwa familia mbalibali.