BURUNDI-MAZUNGUMZO

Mazungumzo Burundi: Msuluhishi kukutana na CNARED

Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania.
Picha ya zamani inaonyesha Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Desemba 9, 2005, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya uhuru wa Tanzania. © MWANZO MILLINGA / AFP

Baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mgogoro nchini Burundi kutokana na uamuzi wa rais wa kuwania muhula wa tatu, msuluhishi kutoka Tanzania, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, alijaribu kufufua mazungumzo ya amani baina ya Warundi yaliyokua yamekwama kwa miezi kadhaa katika kikao kiliofanyika mjini Arusha.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku nne ya kuwasikiliza wadau kutoka pande zote zilizokua ziliitishwa katika kikao hiki, mambo yameanza kueleweka, ingawa bado kuna mambo mengi ya kufanya. Jumanne, Mei 24, wakati wa sherehe za kuhitimisha kikao hicho cha mazungumzo ya amani, hakuna tangazo la kuvutia lililotolewa, lakini msuluhishi ameahidi kukutana kwa mara nyingine katika wiki zijazo.

Ndani ya siku kumi na nne, Rais wa zamani wa Tanzania na msuluhishi katika mgogoro wa Burundi, Benjamin Mkapa, atakutana na "wale ambao hawakuweza kuja kushiriki katika kikao hiki." Itafahamika kwamba muungano unaojumuisha vyama vikuu vya upinzani na wanasiasa vigogo waliojiondoa kutoka chama tawala CNDD-FDD (CNARED), haukualikwa kushiriki kikao hiki kiliyofanyika mjini Arusha kwa sababu ya kupingwa na serikali ya Burundi.

Baadhi ya wanasiasa kutoka muungano huo, hatimaye, walishiriki kikao hiki mjini Arusha, licha ya wito wa kukisusia uliyotolewa na CNARED. Hata hivyo, Benjamin Mkapa anatarajiwa kukutana na CNARED pamoja na vyama vikuu vya kiraia vilioongoza maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza na ambavyo vilikimbilia uhamishoni, kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na timu ya upatanishi.

Kisha msuluhishi atapanga, na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, mpatanishi mkuu, namna ya kutatua mgogoro nchini Burundi, kabla ya maandalizi ya kikao kipya cha mazungumzo kwa minajalli ya kurejesha amani nchini humo, katika wiki ya tatu ya mwezi Juni. Shughuli hiyo inaonekana kuwa itakuwa ngumu zaidi kuliko kikao cha kwanza, kwa sababu Benjamin Mkapa atajaribu kutokuwa na upendeleo kwa kupatanisha pande mbili hasimu juu ya kushiriki mazungumzo, ajenda ya mazungumzo au nchi ambayo itakua mwenyeji wa mazungumzo yajayo.

Wazo linalotazamiwa kufuata mkondo wake: kuidhinisha mpango na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Inasemekana kuwa huenda Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaweza kuzilazimisha pande zote kushiriki mazungumzo ya amani.