KENYA-ULAYA

Nchi za Ulaya zalaani mauaji ya waandamanaji Kenya

Askari polisi akimpia mmoja wa waandamanaji katika jengo moja wakati wa maandamano mjini Nairobi, Kenya, Mei 16, 2016.
Askari polisi akimpia mmoja wa waandamanaji katika jengo moja wakati wa maandamano mjini Nairobi, Kenya, Mei 16, 2016. REUTERS/Goran Tomasevic

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya na Marekani wanaowakilisha nchi zao nchini Kenya wamelaani mauaji na majeraha waliyoyapata waandamanaji siku ya Jumatatu wakati wa maandamano ya upinzani kuwashinikiza Makamishena wa tume ya uchaguzi kujiuzulu kuelekea Uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Mabalozi hao wasema machafuko hayatasaidia lolote na badala yake wanatoa wito kwa serikali na upinzani kuja katika meza ya mazungumzo ili kulizungumzia suala hili la tume ya uchaguzi.

Aidha, wametaka serikali kuchunguza na kuwachukulia hatua maafisa wa polisi waliotumia risasi za moto kuwashambulia waandamanaji Magharibi mwa nchi hiyo.

Maandamano mengine yatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu wiki ijayo ikiwa mwafaka hautafikiwa.