KENYA-UPINZANI

Serikali ya Kenya kuwachukulia hatua viongozi wa upinzani

Serikali ya kenya imetishia kuwatia nguvuni viongozi wa upinzani nchini humo ikiwa watakuwa na mkutano wa hadhara siku ya Jumatano wiki hii.

Askari polisi akimpiga mmoja wa waandamanaji wakati wa maandamano Nairobi Mei 16, 2016.
Askari polisi akimpiga mmoja wa waandamanaji wakati wa maandamano Nairobi Mei 16, 2016. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Itakuwa ni siku ya Kenya kaudhimisha siku ya Madaraka na kumekuwa na mabishano makali kuhusu upinzani kutumia bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi.

Wiki karibu tatu, upinzani nchini Kenya umekua ukiandamana, ukiomba maafisa wa Timu ya Uchaguzi waondolewe kwenye nyadhifa zao kutokana na kuonyesha upendeleo kwa chama tawala nchini humo.

Maandamano ya hivi karibu yalisababisha watu kadhaa kuuawa, wengine kujeruhiwa na wengine kukamatwa.

Hata hivyo maafisa wa Tume ya Uchaguzi, hivi karibuni waliapa kutojiuzulu kwenye nafasi zao.

Watu wengi nchini Kenya wamekua na hofu ya kutokea hali kama ile iliyoshuhudiwa, baada ya uchaguzi uliyotangulia.