Rais Museveni kulihutubia taifa
Imechapishwa:
Rais wa Uganda Yoweri Museveni leo atalihutubia taifa kupitia bunge kueleza mikakati yake ya miaka mitano ijayo baada ya kuapishwa hivi karibuni kuendelea kuongoza nchi hiyo.
Hotuba hii inakuja baada ya wabunge kuapishwa huku wananchi wa Uganda wakiwa na matarajio makubwa.
Hayo yakijiri Rais wa Korea Kusini Park Guen-Hye anayezuru nchini Uganda, amekubaliana na mwenyeji wake Yoweri Museveni kusaidia kuimarisha kiwango cha kilimo vijijini.
Rais Museveni amesema mpango huu utasaidia nchi yake kuimarika kiuchumi kama ilivyo kwa Korea Kusini na watalaam wa nchi hiyo watakwenda nchini Uganda kuwasaidia wakulima.
Korea Kusini imetoa msaada wa Shilingi za Uganda Bilioni 9 kufanikisha mradi huo.
Kuhusu suala la silaha za Nyuklia serikali ya Uganda imesisitiza kuachana kabisa na ushirikiano wake na Korea Kaskazini nchi ambayo imekuwa ikishtumiwa kuhatarisha usalama wa dunia kwa kuendelea kujaribu silaha zake.